Waziri wa nchi ofisi ya Raisi menejimenti ya Utumishi wa umma Hawa Ghasia amekanusha madai kuwa tatizo la mimba kwa wanafunzi mkoani mtwara linachangiwa na mila ya unyago.
Alikuwa akizungumza kwenye baraza la Idd la wanawake wa mkoa wa mtwara katika shule ya sekondari ya seminari ya kiislamu ya midese mkoani mtwara.
Waziri alisema tatizo la mimba kwa wanafunzi mkoani mtwara halichangiwi na unyago kama wengi wanavyodai, bali linachangiwa na wazazi wa sasa kutowatunza na kuwalea watoto wao katika maadili mema, yanayoendana na imani zao.
"katika vitu ambavyo vinanitia aibu hata tunapokuwa katika baraza la mawaziri ni mimba za wanafunzi, wanasema unyago unachangia, lakini mimi nawaambia unyago hauhusiki katika hili, kama tatizo ni unyago mbona sisi tumechezwa na hakukua na tatizo hili?" Alihoji waziri.
Alisema kuwa unyago si mila iliyoibuka hivi siku za hivi karibuni bali ni ya mababu zetu na wakati huo tatizo la mimba kwa wanafunzi halikuwapo, hivyo si kweli kudai kuwa tatizo la mimba mkoani mtwara linachangiwa na unyago.
Ghasia alitumia fursa hiyo, kuwataka wazazi kuwa mfano bora wa kuigwa na watoto katika malezi na makuzi yao ili kuwalinda na changamoto za maisha zinazowakabili hivi sasa.
Haya mmesikia maneno ya mama? Vidume hebu acheni wanafunzi wasome kwanza, na nyinyi mabinti tulizeni boli kwanza someni, wanaume mtawakuta mbele ya safari, elimu kwanza!!!!
Thursday, September 24, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment