Thursday, September 24, 2009

Siri ya miwani ya mwigizaji jim Iyke yafichuka.

Imegundulika kuwa mwigizaji nyota wa filamu za kinaijeria Jim Iyke anavaa miwani myeusi muda wote eti ni kwa vile ana aibu na hana ujasiri wa kusimama mbele za watu na kujieleza.
Siri hiyo imevujishwa na rafiki yake wa karibu wiki iliyopita na alipoulizwa Jim mwenyewe alikiri bila kificho kwamba miwani hiyo ndio kinga yake.
"Asili yangu ni mtu mwenye aibu kusimama mbele za watu wengi ndio maana napendelea kuvaa miwani ya jua hata kwenye mazingira ambayo hayastahili." Alisema.
"Ile miwani inanisaidia kuficha mambo mengi, watu wengi hawatambui kama mimi nina aibu ndio nakuambia kwa mara ya kwanza. Ni ngumu kuniona sehemu yoyote bila miwani yangu iwe usiku au mchana. Najivunia sana mambo yangu binafsi ndio maana watu walikuwa hawalijui hili la miwani."
"Kwanza sinywi kwenye baa za hovyo, sichanganyiki na wasanii mara nyingi ma hata nikiwa nao siwezi kusema mambo yangu. Gari zangu zote zina vioo vyeusi, nimeshinda tuzo nne mpaka sasa sijawahi kuhudhuria hafla hata moja. Zote huwa natuma mtu, yote sababu ya aibu, lakini hakuna aliyekuwa akilijua hilo." Ndivyo alivyomaliza nguli huyu wa kinaijeria.

No comments:

Post a Comment