Thursday, September 24, 2009

Juliana afukuzia Uraia wa Canada.


Msanii nyota wa kike wa miondoko ya taratibu raia wa Uganda, Juliana Kanyomozi, ameripotiwa kuwa katika harakati za kuupata uraia wa Canada ili aweze kujipatia nafasi ya kusoma nchini humo.

Habari zilizopatikana kutoka mjini Kampala, zinasema kuwa tayari mipango ya kuhakikisha mwanadada huyo anachukua uraia wa Canada imeshaanza kufanyika miezi michache iliyopita huku binamu yake aishiye nchini humo aliyefahamika kwa jina la Ruhweza ambaye kwa hivi sasa anaishi nchini Canada akiwa muunganishaji wake.

Ndugu huyo wa Juliana tayari ameshaanza kuchukua vielelezo vya Juliana pamoja na wanawe ili kuhakikisha mwanamuziki huyo anapata uraia wa Canada.

Hata hivyo imeelezwa kuwa, Juliana ana mpango wa kuachana na muziki na kujishughulisha zaidi na masuala ya biashara kati ya Uganda na Canada.

No comments:

Post a Comment