Mshindi wa kombe la dunia akiwa na Brazil, Romario de Souza amedhamiria kuwania kiti cha bunge la msimu ujao.
Romario anakabiliwa na tatizo kubwa la madeni na tuhuma za ufisadi.
Mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 43 ambaye alifunga mabao 70 katika mechi 80 akiwa na Brazil alikuwa katika kikosi cha ushindi cha mwaka 1994.
Amedhamiria kujiunga na chama cha kisoshalisti katika uchaguzi wa mwaka 2010 wa serikali za shirikisho limeeleza gazeti la O Globo la nchini Brazil.
"Romario atakuwa na sera zake na hawezi kutegemea kura za mashabiki wake," alieleza msemaji wa chama hicho katika jimbo la Rio ambaye pia ni mwenyekiti, Alexandre Cardos.
Mwezi Agosti,Romario, ambaye anakabaliwa na tatizo la kukwepa kodi, pia anatuhumiwa kwa kujiingiza katika kamari kinyume cha sheria, tuhuma hizo zinachunguzwa.
Pia alilazimishwa kuuza nyumba yake ya kifahari mjini Rio De Janeiro ambayo ilimwezesha kupata dola milioni 4.37.
Fedha zote za faida ya mauzo hayo na kamari zilikamatwa kwa amri ya mahakama hadi alipe fedha zote anazodaiwa.
Romario alizichezea PSV Eindhoven na Barcelona na alistaafu akiichezea Vasco De Gama mwaka 2008.
Thursday, September 24, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment