Wednesday, September 30, 2009

Pilika za mabinti wa Kibongo!

Huyu mwanada juu hapa anaitwa Hawa. Kwa wapenzi wa Muvi za kibongo, ni mmoja kati ya wacheza muvi wa mwanzoni kabisa kibongo bongo. Alicheza muvi moja inayoitwa masaa 24 na ikashika sana kibongo bongo enzi hizo kabla ya kutokomea zake ulaya kupiga michakato mingine ya maisha. Sasa je ana mipango mingine ya kurudi kwenye gemu au kaja kuvuta hewa tu? Welcome Bongo Sister, Msalimie Omari Gwala.!!
Ndani ya bonge la miwani na hereni kubwa, juu full gold nywele, wenyewe wanaita sijui bleach. Huyu mwanadada anaitwa Shaa au jina lake halisi anaitwa Sara Kaisi. Ndio kati ya mshindani wa MTV Music awards zitakazofanyika kule mjini Nairobi akiiwakilisha vema Tanzania. Mwanzoni alizoeleka na Style yake ya nywele ya kukata upande mmoja na kuzilaza upande mwingine, now kaja na style mpya, hebu mchekini kwenye hiyo picha hapo juu, halafu mtajaji wenyewe Style ipi ni bomba zaidi? Hii au ile ya awali.

Jinsi vipodozi vilivyomkomesha Wema Sepetu!!

Kaika katiza katiza yangu mitaani nilikuta kina dada fulani wakimzungumzia Wema Sepetu kwamba ameanza kuharibika ngozi vibaya mno kisa kutafuta rangi nyeupe kwa nguvu, kwa vikorombwezo vikali either kwa minajili ya kujichubua au kujin'garisha. Basi nikasema ngoja nikaperuzi huku na kule kupata ukweli wa stori hiyo. Bahati nzuri sana nikafanikiwa kupata picha hizi kwa hisani kubwa ya Global Publishers. Cheki picha ya juu, uso kama unataka kuwa na rangi mbili hivi wekundu na weupe, na kwa kweli ukiitizama kwa ukaribu utagundua imepoteza hali ya kun'gaa. Cheki mkono ni kama unataka kupata mipasuko hivi. Picha ya Chini ndio duu inatisha, cheki miguu. Dada Zetu mbona mmeumbwa fresh mnataka nini tena kwenye mavipodozi makali tena yaliyopigwa marufuku? Haya wajemeni ipo siku tutasikia pua zimeanza kumon'gonyoka na kudondoka. Pole dada Yangu Wema!!!


Tuesday, September 29, 2009

Pilika Za Mastaa wetu!!

Kwa wale wapenzi wa filamu kazi kwao, mtaalamu wa muvi za kibongo Kanumba ameibuka na filamu nyingine mpya inayokwenda na jina Village Pastor. Muvi imeingia dukani jana jumatatu tarehe 29 september. Katafute kopi yako upate uhondo wa mtaalamu kanumba a.k.a The Great!!!
....................................................................................................................................
....................................................................................................................................

Mwanadada hapo juu anaitwa Salama Jabiri, jaji wa Bongo Star Search na ni mtangazaji wa East Africa Radio na Tv.Ni maarufu miongoni mwetu hususan wana burudani. Huyu mdada bwana anapenda style fulani za kuvaa kisela kama kiume hivi, lakini hebu mcheki katika new look yake hapo. Cheki style yake ya nywele katoka full kidada au sio!
.........................................................................................................................
.................................................................................................................

Mwanada anaitwa Beyonce Knowles a.k.a mama Jay Z. Huyu mwana dada bwana ni bonge la sister duu namaanisha mzuri kwa sura na umbo pia, but angalia vizuri picha zake zote nne hizo za juu na chini umegundua nini? Mimi nilichokigundua ni kwamba mwanadada ni kama amefanyiwa upasuaji kuongezea urembo wake. Tazama picha mbili za juu, hizo inaonyesha alifanya upasuaji wa pua kama kuichonga hivi. Picha ya kushoto mgongo wa pua unaoonekana mpana, wakati ya kushoto ni baada ya kuichonga pua yake kiasi kwamba mgongo wa pua umeonekana kuchongwa vyema na kuwa mwembamba. Picha ya chini angalio tofauti ya maziwa yake. Wakati ya kushoto anaonekana alikuwa na maziwa madogo tu ya kawaida, ya kulia ana kitu "baloon" hapa namaanisha lazima alipitia kwa daktari kuongeza ukubwa wa matiti. Kazi kwenu warembo!!!!!
.................................................................................................................
.................................................................................................................




Monday, September 28, 2009

Big Brother Afrika yachanja mbuga!!

Kama kawaida ya Big Brother Africa ya kila mwaka, masuala ya mapenzi taratibu yameanza kuchukua nafasi. Pichani washiriki Liz na Kevin wakiwa wamejipunzisha ndani ya shuka wakibadilishana stori taratiiiibu!!!

Na huyu mdada pia ni mshiriki wa Big Brother anaitwa Jennifer lakini ameustua ulimwengu baada ya kumwambia msimamizi wa Big brother kuwa anataka kujitoa shindanoni kwa hiari yake mwenyewe. Hajaeleza wazi kwa nini ameamua kujitoa, lakini inahisiwa kuwa ni mjamzito kwani kwa siku kadhaa amekuwa akilalamika kuwa anaumwa. Lakini pia inahisiwa ana matatizo ya kifamiia nyumbani kwao, matatizo ambayo yanaonekana kumuathiri kisaikolojia kiasi cha kumlazimisha kujitoa. Pole kwake!

Friday, September 25, 2009

Tulonge kidogo kuhusu Burudani za Kibongo.

Huyu ndio mwanadada Dj Fetty, Dj maarufu sana nchini Tanzania akipiga mzigo katika kituo cha Radio cha Clouds Fm na mara nyingi utamsikia katika kipindi cha XXL cha B12 Jtatu mpaka ijumaa, na pia utampata katika kipindi cha Bongo flavour kila jumamosi. Tuache utani, namfeel kideadly mwanadada huyu linapokuja suala la utangazaji na deejaing. Anajua kutangaza na mpangilio wake wa maneno ni wa hali ya juu. Big up Kwake!!!
Kwa wale wanaofuatilia Maisha Plus, Auditions zinaendelea katika mikoa tofauti tofauti tayari kwa kupata washiriki watakaoingia kule kijijini tayari kuanza maisha magumu ya kijijini kuusaka mshiko na kumvua ubingwa Abdul mshindi wa shindano lililopita aliyetokea Zanzibar. Kama vipi kina Masoud Kipanya(Pichani juu) wakipita maeneo yenu jitokezeni kwa wingi huwezi jua bwana unaweza ukajikuta unawin mahela.
Na ule Utamaduni wa kila mwaka unaoshika na kubamba kila mwaka wa kukutana na kula shangwe za maana, umekuja tena. Hapa nazungumzia Fiesta. Kila mwaka utamaduni huu uja na kauli mbiu yake, wakati mwaka jana ilikuwa full shangwe, mwaka huu ni "One love". Mwaka huu Tamasha litaanzia mkoani Dodoma kwa wasanii mbalimbali kutumbuiza, list ya wasanii ni ndefu lakini nitakutajia wachache. Atakuwepo Mangwea, Marlaw, Quick Rocka, Mr Blue, Cege, Temba, Fid Q, Cyrill, Niki wa Pili, Suma Lee, Maunda Zorro, Chiku, Jos Mtambo na wengine wengi.
Mara zote tamasha hili huzunguka mikoa mbali mbali na kumalizikia Dar Es Salaam ambako huwa kuna msanii mkubwa wa kimataifa hutumbuiza, je mwaka huu atakuja nani? Stay tuned.
Dogo hapo juu anaitwa Stan Boy, msanii wa Bongo Flavour. Kwa habari za juu juu nilizopata, ni kwamba bwana mdogo amefungua Studio yake ikiwa na maana ni One step ahead. Alikuwa kimya muda mrefu kwenye michongo ya shule na vitu kama hivyo lakini he is back na ana single yake mpya inayoitwa Take You Out. Kwa anayejua muziki najua hatonibishia nikisema kwamba ni bonge la R&B!! Welcome back, Stan Boy. Na kama kweli amefungua studio, big up sana kwake.



Thursday, September 24, 2009

Ray aja na Taswira.


Msanii nguli wa filamu hapa nchini, Vicent Kigosi almaarufu Ray anatarajia kutoa filamu kali ya aina yake inayokwenda kwa jina la Taswira.

Msemaji wa kampuni ya Shariff Production inayoandaa filamu hiyo, Shariff Jumbe amesema Ray amecheza kama kaka fuska, ambaye anaangukia kwenye penzi la dada yake bila kujijua.

Filamu hii imeshirikisha mastaa wengine kama akiwmo Charles Magari'mzee magari', Hidaya Njaidi'mama Tunu', Juma Chikoka'chopa', na Ruyu.

Kwa sasa ndio ametoka kuingiza sokoni filamu yake nyingine inayokwenda kwa jina DIVORCE na pia stay tuned kwa filamu yake nyingine inayoitwa Fair Decision.

Mabomu Tena Mbagala!!!

Mabomu mengine yamelipuka jana tar 24 sept jirani na kambi ya jeshi la Wananchi (JWTZ), iliyopo mbagala kizuiani, na kusababisha vifo vya watoto wawili Regina Chawele(5) na Rajab Said(6), na pia kujeruhi vibaya wengine watano.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo la jana, linadaiwa kutokea majira ya saa mbili asubuhi.
Pole kwa mliofikwa na msiba, na muugue pole wote mliojeruhiwa.

Miss Tanzania 2009 Yazidi kunukia.


Kisura wa Tanzania katika shindano la miss Tanzania anategemea kujulikana tarehe 2/10/2009 katika ukumbi wa Mlimani City.
Shindano hilo linaloandaliwa kila mwaka na Lino International Agency chini ya Hashim Lundenga, mwaka huu linategemea kushirikisha warembo 30 kutoka mikoa mbali mbali nchini Tanzania.
Warembo hao kwa sasa wameweka kambi katika Hotel ya Giraffe View Oceanic iliyoko maeneo ya kunduchi tokea tar 7 Sept 2009.
Mshindi wa taji hilo anategemea kutoka na zawadi ya gari lenye thamani ya Tsh milioni 45 pamoja na fedha Taslimu Tsh milioni 9 vyote vikiwa na jumla ya Tsh milioni 54.
Taji hilo kwa sasa linashikiliwa na Nasreem Karim.

Mercy Johnson Apania kuolewa!

Binti muigizaji wa kinaijeria mwenye mvuto na mafanikio makubwa katika tasnia ya filamu za kinaijeria, Mercy Johnson, amesisitiza kwamba lazima aolewe mwaka huu na akasema atakayemuoa lazima awe mkristo kama yeye.
"Kuna wanaume wengi sana wananifuatilia na wanataka kunioa lakini inabidi niwe makini sana ndio maana nawachorea mstari ambao nawataka nawaweka upande mmoja na wengine pembeni." Alisema.
"Mwanaume atakayenioa mimi ni lazima awe na fedha kwanza, anayemuogopa Mungu, mrefu na mzuri kwa sura. Lazima awe mkweli na ambaye anaweza kunitatulia tatizo lolote."
Msanii huyu ambaye anadai alizaliwa miaka 24 iliyopita, amekuwa akikumbwa na kashfa kila kukicha na ni miongoni mwa wasanii maarufu sana wa Nollywood.

Mtanzania Bingwa wa kukata viuno ndani ya Big Brother

Mshiriki mtanzania katika shindano la Big Brother, Elizabeth Gupta amekuwa kivutio kwa mwenzake kutokana na uwezo mkubwa wa kukata mauno.
Washiriki wenzake wamekuwa wakimsifia kutokana na uwezo ambao amekuwa akiuonyesha kwa kukata mauno kila unapopigwa muziki hasa ule ulio katika miondoko ya kuchezeka.

"mimi napenda sana kucheza, nataka nijiendeleze katika sanaa hadi katika ngazi ya chuo kikuu." Alisema Alizabeth wakati akiwaeleza wenzake.

Washiriki hao wamekuwa wakikaa pamoja na kucheza kwa zamu kila mmoja akionyesha uwezo alionao katika fani hiyo, na Elizabeth amekuwa kati ya kivutio kikubwa kwa wenzake.

Juliana afukuzia Uraia wa Canada.


Msanii nyota wa kike wa miondoko ya taratibu raia wa Uganda, Juliana Kanyomozi, ameripotiwa kuwa katika harakati za kuupata uraia wa Canada ili aweze kujipatia nafasi ya kusoma nchini humo.

Habari zilizopatikana kutoka mjini Kampala, zinasema kuwa tayari mipango ya kuhakikisha mwanadada huyo anachukua uraia wa Canada imeshaanza kufanyika miezi michache iliyopita huku binamu yake aishiye nchini humo aliyefahamika kwa jina la Ruhweza ambaye kwa hivi sasa anaishi nchini Canada akiwa muunganishaji wake.

Ndugu huyo wa Juliana tayari ameshaanza kuchukua vielelezo vya Juliana pamoja na wanawe ili kuhakikisha mwanamuziki huyo anapata uraia wa Canada.

Hata hivyo imeelezwa kuwa, Juliana ana mpango wa kuachana na muziki na kujishughulisha zaidi na masuala ya biashara kati ya Uganda na Canada.

Huyu ndiye mwenye Blog hii!!

Anaitwa John Mabula, umri miaka 29, mkazi wa Dar Es Salaam. Ni mpembuzi makini wa masuala mbalimbali ya mambo ya kijamii, burudani, michezo na michapo ya kitaa. Tegemea mengi toka kwake.


Romario sasa adhamiria kuwa mwanasiasa.

Mshindi wa kombe la dunia akiwa na Brazil, Romario de Souza amedhamiria kuwania kiti cha bunge la msimu ujao.
Romario anakabiliwa na tatizo kubwa la madeni na tuhuma za ufisadi.
Mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 43 ambaye alifunga mabao 70 katika mechi 80 akiwa na Brazil alikuwa katika kikosi cha ushindi cha mwaka 1994.
Amedhamiria kujiunga na chama cha kisoshalisti katika uchaguzi wa mwaka 2010 wa serikali za shirikisho limeeleza gazeti la O Globo la nchini Brazil.
"Romario atakuwa na sera zake na hawezi kutegemea kura za mashabiki wake," alieleza msemaji wa chama hicho katika jimbo la Rio ambaye pia ni mwenyekiti, Alexandre Cardos.
Mwezi Agosti,Romario, ambaye anakabaliwa na tatizo la kukwepa kodi, pia anatuhumiwa kwa kujiingiza katika kamari kinyume cha sheria, tuhuma hizo zinachunguzwa.
Pia alilazimishwa kuuza nyumba yake ya kifahari mjini Rio De Janeiro ambayo ilimwezesha kupata dola milioni 4.37.
Fedha zote za faida ya mauzo hayo na kamari zilikamatwa kwa amri ya mahakama hadi alipe fedha zote anazodaiwa.
Romario alizichezea PSV Eindhoven na Barcelona na alistaafu akiichezea Vasco De Gama mwaka 2008.

Waliomuua albino wahukumiwa kunyongwa.

Mahaka kuu maalumu mjini Kahama mkoani shinyanga imewahukumu kunyongwa hadi kufa watu watatu baada ya kupatikana na hatia ya kosa la mauaji ya kukusudia ya mtoto mwenye ulemavu wa ngozi(albino) Matatizo Dunia(13) mkazi wa Bunyihuna Bukombe.
Waliohukumiwa kutumikia adhabu hiyo ni Bw. Masumbuko Mada(32), Bw.Emmanuel Masangwa(28) na Charles Masangwa(42).
Akiwasomea hukumu yao, Jaji Gabriel Rwakibalila alisema ametoa hukumu hiyo ya kunyongwa hadi kufa kwa washitakiwa hao watatu baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka kuwa washitakiwa walitenda kosa hilo.
Kwa kuzingatia ushahidi huo Jaji Rwakibalila aliwapa hukumu hiyo kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai 196 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 na hata hivyo alisema wanayo nafasi ya kukata katika mahakama ya juu iwapo watakuwa hwakuridhika na hukumu hiyo.

Siri ya miwani ya mwigizaji jim Iyke yafichuka.

Imegundulika kuwa mwigizaji nyota wa filamu za kinaijeria Jim Iyke anavaa miwani myeusi muda wote eti ni kwa vile ana aibu na hana ujasiri wa kusimama mbele za watu na kujieleza.
Siri hiyo imevujishwa na rafiki yake wa karibu wiki iliyopita na alipoulizwa Jim mwenyewe alikiri bila kificho kwamba miwani hiyo ndio kinga yake.
"Asili yangu ni mtu mwenye aibu kusimama mbele za watu wengi ndio maana napendelea kuvaa miwani ya jua hata kwenye mazingira ambayo hayastahili." Alisema.
"Ile miwani inanisaidia kuficha mambo mengi, watu wengi hawatambui kama mimi nina aibu ndio nakuambia kwa mara ya kwanza. Ni ngumu kuniona sehemu yoyote bila miwani yangu iwe usiku au mchana. Najivunia sana mambo yangu binafsi ndio maana watu walikuwa hawalijui hili la miwani."
"Kwanza sinywi kwenye baa za hovyo, sichanganyiki na wasanii mara nyingi ma hata nikiwa nao siwezi kusema mambo yangu. Gari zangu zote zina vioo vyeusi, nimeshinda tuzo nne mpaka sasa sijawahi kuhudhuria hafla hata moja. Zote huwa natuma mtu, yote sababu ya aibu, lakini hakuna aliyekuwa akilijua hilo." Ndivyo alivyomaliza nguli huyu wa kinaijeria.

Waziri asema unyago hauchangii mimba!

Waziri wa nchi ofisi ya Raisi menejimenti ya Utumishi wa umma Hawa Ghasia amekanusha madai kuwa tatizo la mimba kwa wanafunzi mkoani mtwara linachangiwa na mila ya unyago.
Alikuwa akizungumza kwenye baraza la Idd la wanawake wa mkoa wa mtwara katika shule ya sekondari ya seminari ya kiislamu ya midese mkoani mtwara.
Waziri alisema tatizo la mimba kwa wanafunzi mkoani mtwara halichangiwi na unyago kama wengi wanavyodai, bali linachangiwa na wazazi wa sasa kutowatunza na kuwalea watoto wao katika maadili mema, yanayoendana na imani zao.
"katika vitu ambavyo vinanitia aibu hata tunapokuwa katika baraza la mawaziri ni mimba za wanafunzi, wanasema unyago unachangia, lakini mimi nawaambia unyago hauhusiki katika hili, kama tatizo ni unyago mbona sisi tumechezwa na hakukua na tatizo hili?" Alihoji waziri.
Alisema kuwa unyago si mila iliyoibuka hivi siku za hivi karibuni bali ni ya mababu zetu na wakati huo tatizo la mimba kwa wanafunzi halikuwapo, hivyo si kweli kudai kuwa tatizo la mimba mkoani mtwara linachangiwa na unyago.
Ghasia alitumia fursa hiyo, kuwataka wazazi kuwa mfano bora wa kuigwa na watoto katika malezi na makuzi yao ili kuwalinda na changamoto za maisha zinazowakabili hivi sasa.
Haya mmesikia maneno ya mama? Vidume hebu acheni wanafunzi wasome kwanza, na nyinyi mabinti tulizeni boli kwanza someni, wanaume mtawakuta mbele ya safari, elimu kwanza!!!!

Kutovuta sigara kwapunguza tatizo la moyo.

Upigaji marufuku uvutaji wa sigara katika maeneo ya umma kumeonekana kuleta mafanikio makubwa katika uzuiaji wa maradhi ya shambulio la moyo kuliko ilivyotarajiwa, takwimu mpya zimeonyesha.
Upigaji marufuku uvutaji sigara umepunguza idadi ya kesi za mashambulio ya moyo barani ulaya na amerika ya kusini kufikia theluthi moja, kwa mujibu wa ripoti mbili tofauti.
Ripoti ya utafiti huo ilionekana katika majarida maarufu ya circulation na jarida la chuo cha kati cha maradhi ya moyo cha marekani.
Mashambulio ya moyo nchini uingereza pekee huathiri watu 275,000 na kuua 146,000 kila mwaka. Mapema mwezi huu ilitangazwa kwamba kiwango cha shambulio la moyo kwa mwaka kilianguka kwa asilimia 10 nchini uingereza baada ya kupiga marufuku uvutaji sigara maeneo ya umma julai 2007, kikiwa kiwango kikubwa zaidi ya kile kilichotarajiwa.
Haya wabongo, na sisi lini tutapiga marufuku uvutaji wa sigara hadharani???

Wednesday, September 23, 2009

John mabula naye ndani ya Blog!!

John Mabula naye ndani ya Blog!!! Kwa wale wanaonifahamu au wasionifahamu, haijalishi lakini ukweli ni kwamba ndio naingia rasmi mwanaharakati wa mambo ya maisha, vijana, burudani, michezo, maisha ya mapenzini na michapo ya kitaa. Stay tuned!!