Thursday, October 1, 2009

Jamaa South Africa aoa wanawake wanne Kwa mpigo.

Njemba moja nchini Afrika kusini ametoa kioja cha mwaka kilichostua na kushangaza dunia baada ya kuoa wanawake wanne kwa mpigo. Jamaa huyo anayeitwa Milton mbele ambaye ni mtu mzito tu mwenye pesa zake, anasema amefanya hivyo ili kupunguza gharama ya kuoa tofauti tofauti na hivyo kupunguza kugharamia sherehe tofauti tofauti.
Alipoulizwa aliwezaje kuwashawishi mabinti hao kukubali kupanda katika altare moja kufunga ndoa alijibu kwa ufupi tu, "its just a matter of negotiation." Yaani alikaa na wanawake zake wote wanne, akaongea nao na wakakubaliana bila tabu.
Utamaduni wa kuwa na wake wengi ni wa kawaida kabisa hususani Afrika, lakini hii ya kuoa wote kwa mpigo ni mpya na kali.
Majina ya wake zake hao ni Smangele cele, Thobile vilakazi, Zanele Langa na Happiness Mdlolo.

Hebu Imagine unatinga zako St. Peters au St Joseph namna hii, umeshika wasichana zako unataka kupanda nao Altareni kufunga ndoa, si watakutoa mbio kinoma!! Lakini kwa Madiba mambo mswano mwenzenu huyo na maharusi wake wakitinga church!!

No comments:

Post a Comment