Thursday, October 1, 2009

Habari za hivi karibuni zinasema, msanii maarufu Justin Timberlake kutoka nchini marekani anategemea kuwasili nchini hivi karibuni kwa ajili ya kupanda mlima kilimanjaro akiongozana na mpenziwe ambaye ni mcheza muvi mashuhuri wa Hollywood Jesicca Biel, ikiwa ni sehemu ya kukusanya pesa kwa ajili ya kusaidia tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama duniani.
Hiyo itakuwa ni ziara ya pili kwa siku za karibuni kwa mastaa wa dunia kuja kupanda mlima kilimanjaro kwani siku kadhaa zilizopita bilionea wa kirussia ambaye pia ni mmiliki wa timu ya mpira ya Chelsea ya uingereza, alikuwepo pia nchini kupanda mlima huo.
Vile vile kuna habari kuwa msanii mkongwe wa nchini marekani bibie Madonna naye pia huenda akaja kwa ajili ya zoezi hilo hilo la kuupanda mlima kilimanjaro, the second largest mountain in the world.
Watanzania lazima tujivunie urithi wetu au sio, si unaona mastaa wanavyopigana vikumbo kuja kuupanda!!
....................................................................................................

Mpenzi wa muigizaji mahiri wa nchini marekani(Hollywood), mkongwe Mel Gibson, bibie Oksana Grigorieva amesema kuwa sasa hivi anafikiria zaidi mambo yake ya muziki na jinsi atakavyomlea mtoto wake mtarajiwa, na hafikirii ndoa hata kidogo. Oksana ni mjamzito kwa sasa na anategemea kujifungua mwezi December.

Hayo ameyatamka mwenyewe wakati akihojiwa katika TV ya GMTV chini ya mtangazaji Lorraine Kelly. "Hatuna mpango wa kufunga ndoa kwa sasa." Alijibu swali la mtangazaji huyo aliyeuliza kuzagaa kwa umbeya kuwa amevishwa pete ya uchumba na Mel Gibson, baba mtarajiwa. "Sijawahi kabisa kukaa na kufikiria suala la ndoa." Alihitimisha mwana mama huyo wa miaka 39 ambaye tayari ana mtoto mwingine wa miaka 12 aliyemapata katika mahusiano yake ya awali na mwanaume mwingine. (Du!! Wabongo huku wanazitafuta ndoa, mwenzetu huyu anakomaa hataki ndoa,kama vipi mzee mzima Mel Gibson si aje Bongo tu ajichagulie chake ili aoe fasta!)

No comments:

Post a Comment