Thursday, October 29, 2009

Mambo Mamboz!!

IRENE UWOYA AREJEA BONGO NA MUONEKANO MPYA!
(Picha ya juu ndio muonekano mpya wa Irene Uwoya baada ya kurejea juzi Bongo kwa mapumziko mafupi kutokea nchini Cyprus anapoishi na mumewe. Picha za chini ni za muonekano wake wa zamani)
Jina lake kamili anaitwa Irene Pancras Uwoya, ambaye hivi karibuni tu alifunga ndoa na Hamad Ndikumana, mwanasoka na Raia wa Burundi anayeishi nchini Cyprus akicheza mpira wa kulipwa katika klabu ya daraja la kwanz ya E. Lemosos.
Irene Uwoya ana vipaji kadhaa ikiwemo fani ya urembo na uchezaji wa filamu, akiwa ameshacheza filamu nyingi zilizotamba, na yeye kuzin'garisha vilivyo kama vile Diversion of Love, Hazard, One Blood, Oprah, Mid night, Peace of Mind, Tanzanite, Kalunde na nyinginezo, huku Yolanda ikiwa ndio muvi yake ya kwanza iliyomuingiza kwenye gemu ya filamu.
Katika Tasnia ya filamu ni ukweli usiopingika kwamba Irene ana kipaji cha kuigiza katika mazingira yoyote yale atakayopangwa iwe yale ya uchakaramu, ucheshi, majonzi au vyovyote vile, uwezo uliomfanya apewe tuzo ya muigizaji bora wa kike. Kama unabisha hebu angalia alivyofit kwenye wimbo wa Matonya Tax Bubu, humo ndani aliigiza utafikiri kweli ni malaya wa barabarani haswa.
Mbali ya kufanya vyema kwenye filamu nchini, nyota ya Irene Uwoya ilianza kun'gaa pale alipojiingiza katika mambo ya urembo kwa kushiriki shindano la Miss Chan'gombe ambako alifanikiwa kuwa mshindi wa kwanza, akapata tiketi ya kwenda Miss Temeke, nako akafanya vyema hivyo kwenda moja kwa moja kwenye shindano la Miss Tanzania ambako alifanikiwa kuingia kumi bora na kufanikiwa kushika nambari Tano.

Akiwa ameanza maisha ya mapya ya ndoa sasa, Irene anasema kwamba amejifunza mengi kutokana na ndoa za watu maarufu mbalimbali duniani ambazo ziliyumba na anaamini kikubwa kinachoyumbisha ndoa ni maelewano duni ndani ya nyumba. "Ndoa za mastaa wengi zinavurugika sababu za kutoheshimiana ndani ya nyumba, kila mmoja kutaka kua juu ya mwenzake, watu hawasikilizani. Lakini mimi naahidi siolewi ili niachike, nataka niingie kwenye maisha ya furaha ndani ya ndoa, lakini katika kila jambo ukimtanguliza mungu mbele, mafanikio yatakuwepo.

Hivi sasa Irene yupo nchini kwa shughuli zake binafsi, pamoja na kutengeneza baadhi ya filamu kabla kurejea tena nchini Cyprus anapoishi na mumewe. Ingawa aliporudi tu magazeti ya udaku kama kawaida yalianza kuchombeza, "Vipi mbona karudi, kashaachika nini?" Lakini mwenyewe anasema, "Aaa wapi, nimekuja kwa muda tu?"

.....................................................................

JINI KABULA KAJIWEKA TENA KWA MR. NICE!!
Msanii wa maigizo hapa nchini anayefahamika zaidi kwa jina la Jini Kabula, amemsifu mpenzi wake wa zamani waliyerudiana upya hivi karibuni, Lucas Mkenda,"Mr Nice," kuwa ni mwanaume anayejua mapenzi vilivyo.

Akizungumza kwenye mahojiano na kituo kimoja cha Radio jijini alisikika akisema kuwa tangu warudiane na Mr Nice, baada ya kuachana na baba watoto wake, Tuesday Kihangala "Mr Tues", amekuwa akifaidi mapenzi motomoto toka kwa Mr Nice.

"Kusema kweli Mr Nice amenifanya nimsahau kabisa hata baba watoto wangu Tues, kutokana na mapenzi motomoto anayonipa ikiwa ni pamoja na kunienzi vilivyo." Alisema Jini Kabula aliyejipatia umaarufu mkubwa baada ya kuigiza katika tamthiliya ya Jumba La Dhahabu.

Aidha Kabula alieleza kuwa bado anaendelea kufanya kazi na Mr Tues na hana kinyongo naye na alimuelezea Mr Tues kama mwanaume mcheshi na mwingi wa mizaha kama alivyo yeye. Haya Mambo hao!!

........................................................................

SEMANYA AWAKATA KIDOMO DOMO WANAOSEMA YEYE DUME! Binti aliyezua utata juu ya jinsia yake baada tu ya kushinda mbio za ubingwa wa dunia mita 800 kwa wanawake mjini Berlini nchini ujerumani, Carter Semanya, ameibuka mbele ya ukurasa wa mbele wa jarida maarufu nchini Afrika kusini la YOU akiwa amejiremba kike kike haswa.

Semanya alishinda mbio hizo za ujerumani kwa kutumia dakika 1:55:45 na hivyo kuweka rekodi ya muda wa kasi zaidi kwa mwaka huu, kasi iliyostua ulimwengu na waandaji hasa kasi hiyo ikitoka kwa mwanamke, na hivyo kusababisha afanyiwe uchunguzi kubaini jinsia yake. Hata hivyo Uchunguzi ulionyesha ni kweli Semanya ana homones za jinsia mbili za kike na kiume, lakini yeye anashikilia msimamo kuwa yeye ni mwanamke tu.

Ni kweli ni mwanamke, lakini Du! Vipi hii misuli uliyoitunisha hapa! Hapa ilikuwa siku hiyo ya mashindano hayo ya Berlin.
Alizaliwa miaka 18 iliyopita huko Ga-Masehlong, kijiji kilichopo nchini Afrika kusini karibu na Polkwane kabla ya kwenda kukulia katika iiji kingine cha Fairlie.

Alipokuwa na miaka 14 alifukuzwa kwenye timu ya mpira miguu ya wanawake ya shuleni kwao baada ya kuonekana yuko too Rough wakati akicheza, yaani alikuwa akicheza kama dume, miguvu mingi kwenda mbele, wakaona isiwe tabu wakamuondoa. Hapo ndipo alipoamua kuwa mwanariadha, mchezo uliompa mafanikio na umaarufu huo alionao sasa.

Kwa Sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Pretoria University, akisomea sayansi ya michezo, (Degree in Science of Sports.)

Du! Cheki hili tabasamu lake kwanza baada ya kupokea medali yake ya Dhahabu, Semanya Bwana!!!!!!!

...................................................................
MKE WA BARACK OBAMA AWA GUMZO DUNIANI KWA VIVAZI VYAKE TU, TOFAUTI KABISA NA FIRST LADIES WENGINE!

Hapa akitinga kigauni chekundu, simple kama anaenda dukani vile, kumbe yupo kwenye Red Carpet.
Wala hajali na kigauni chake, utafikiri yuko Mtaani kumbe yupo katika Dhifa ya kitaifa.
Check First Lady Mwenzake suti kali, yeye wala kigauni tu.
Babu wa watu kakaribishwa Ikulu katinga bonge la suti, mcheki yeye kigauni tu!
Katoka Bomba eti eeeeh! Check mguu, mzuri kama wa My lovely Wife.
Bado Simple tu, ila safari hii gauni refu, kaficha guu lake!!
Angalau Yuko Kifirst Lady kidogo, lakini bado, yeye na Suit, NO!
Check kigauni kiko Simple but kimemkaa na kumpendeza. Bibi wa watu kusikia anaitwa ikulu akagonga hiyo sijui inaitwa nini, sijui ni nini.

................................................................

MKIAMBIWA MAPENZI NI UBUNIFU MNAKATAA, CHEKI HAWA!

Bonge la Kiss toka juu ya mti!! Ngoja apatuke huko juu utamu wa mate wote utamtokea puani.
Hawa jamaa bwana, sijui hamu iliwapanda, home wakaona mbali. Ndani ya gari dizaini AC ikawa mbovu, wakaona isiwe tabu ngoja twende kwenye boneti, lakini si wangepaki hata pembeni basi hiyo gari, ndio katikati kabisa! Nina mtoto wangu wa kiume anaitwa Ephraim, ni mtundu sana, but asifikie utundu wa huyu bwana mkubwa hapa juu sijui anachungulia nini kwa binti wa watu, au sijui nao wako katika ubunifu wa mapenzi.

.........................................................

MBONGO ATAMBA ULAYA KWA DESIGNES ZA NGUO. Anayeonekana pichani anaitwa Sheria Ngowi ni mbongo ila yuko pande za ulaya akiwa anafaya shughuli ya kudesign nguo, hapo yeye wenyewe akionyesha kati ya nguo alizozibuni mwenyewe. Tanzania Tutafika Level za kina Calvin Clain very soon si unaona vijana walivyo juu.

..........................................................

MAPACHA WA AJABU CHINI INDIA.

Nchini India kuna mapacha wa ajabu ambao umaarufu wao unaendelea kukua taratibu, labda baada ya kuja kugundua kuwa jinsi walivyo inaweza kuwa dili kwao.

Mapacha hao Ganga na na Jamina ambao wana umri wa miaka 39 sasa, wameungana kuanzia sehemu ya kiuno huku kila mmoja akiwa na mguu mmoja na miguu yao ya pili imeungana na kuform mguu wa tatu ambao wanautumia wote wawili, hii ikiwa na maana wana miguu mitatu kwa ujumla wao.

Daktari mmoja nchini marekani, Dr James Stein, ambaye amespesholaizi katika kufanya operesheni za kutenganisha mapacha walioungana, anadai kuwa anaweza kuwatenganisha ili kila mmoja ajitegemee bila madhara yoyote kutokea,lakini cha ajabu wenyewe wanasema hawataki,kwani hawaoni tatizo lolote la wao kuwa katika hali hiyo.

Wanashangaa watu wanaowashangaa kuwa wao ni viumbe wa ajabu. Wao wanasema wao ni binadamu wa kawaida tu kama wengine na wana hisia kama watu wengine.
Ganga na Jamina, hujiingizia pesa nyingi kutoka kwa watu wanaowalipa ili tu kuwashangaa, pesa wanayoitumia kulisha familia yao ya kimaskini inayofikia watu 22. Du!! Au ndio maana hawataki kutenganishwa, kumbe dili.





















Tuesday, October 13, 2009

Burudani Zaidi!!

TUZO ZA MTV MUSIC AWARDS ZAFANA NAIROBI WIKI HII.
Tuzo za kimataifa za MTV Music Awards ambazo hufanyika kila mwaka huku mwaka huu wana wa East Afrika tulipata bahati ya kuandaa, mjini Nairobi nchini Kenya, wikiendi hii. Picha ya juu Msanii Akon akitumbuiza katika tamasha hilo kama mgeni mwalikwa huku pembeni yake(Mwenye koti jekundu), msanii Wyclef jean naye alikuwepo kutumbuiza.
Picha ya juu wanadada wawili, kushoto ni wa Kundi la Blue 3 la Uganda na kulia ni kutoka Tanzania, mwanamuziki Shaa. Haijaeleweka mara moja hizo nguo walizovaa walipigiana simu wavae sare au bahati mbaya tu waligongana wakiwa sare, maana vijigauni vilifanana kwa kila kitu. Shaa alikuwa akigombea tuzo ya msanii anayechipukia, but alitoka kapa!

Juu msanii Amani kutoka Kenya akiongea kwa furaha baada ya kushinda tuzo ya Best Female Artist from East Africa, akiwapiga bao wasanii kibao wakiwamo Blue 3.

Msanii AY kutoka Tanzania akisalimiana na mashabiki katika Tuzo hizo. AY alikuwa mshindani kuwania Tuzo ya msanii bora wa Hip Hop, ingawa hakufanikiwa kuipata kwani aliyeitwaa ni Dibanj'e kutoka nchini Naijeria.

Kweli majuu hamnazo!! Katika Tamasha hilo msanii Akon na Mwenzake Wyclef walifanya vituko kwa kuanza kuvua nguo jukwaani. Sijui walikuwa wanataka kutuonesha nini, hebu muone Akon(Kushoto) alichokuwa akikifanya huku Wyclef naye suruali ikiwa magotini akimuangalia.
..........................................................................
HAPPINESS MAGESA ACHANJA MBUGA KWENYE MODELLING.Mlimbwende wa kitanzania ambaye pia aliwahi kushikilia taji la Miss Tanzania Happiness Magesa, ambaye kwa sasa anatambulika kwa jina la Millen, amezidi kupaa baada ya sasa kuchukua contract ya kuonyesha mitindo huko New York nchini marekani. Picha ya juu akiwa katika maonyesho yake huko New York. Du!! Hongera zake.
..............................................................................

MERCY ANASEMA MAFANIKIO YAKE HAYAJI KWA UCHAWI.
Uvumi unaoshupaliwa na magazeti ya udaku nchini Naijeria kwamba msanii Mercy Johnson ametoa mimba. Lakini binti huyo mrembo anayependa majigambo, amekanusha vikali na kudai ni majungu ya wasiompenda.
"Nafanya vizuri sana kwenye hii fani na kila mtu anajua. Nimefikia hapa nilipo kutokana na juhudi binafsi kikazi na wala si vitu vingine," alisema. "Mimi juju ya nini? Hainisaidii, yaani nikaloge ili nipate kazi? Hiyo haitapata kutokea wala sijawahi kufikiria kwenda kwa mganga, mimi ni mwenye mtizamo na uelekeo."
"Suala la kutoa mimba, mimi sijawahi kulifikiria, nashangaa hayo maneno yanatoka wapi? Umri wangu ni mdogo sana kufanya mambo kama hayo. Mwenye uthibitisho wa hayo maneno ajitokeze aseme."






Monday, October 12, 2009

Duniani kuna mambo!! Midume yaoana!

Midume miwili nchini Marekani imeamua kufunga ndoa ili kuishi kama mke na mimu kihalali!!! Midume hiyo ni hiyo hapo juu, Jamil na Michael. Kushoto ndio bwana harusi na kulia ndio "Bibi harusi".
Huyu ndio Dume lakini ndio "Bibi harusi wetu akiweka pozi la picha.

Hapa Bibi Harusi akiwa katika pozi na "Matroni zake" wawili.
Picha ya Pamoja ya maharusi na wasindikizaji wa harusi.

Bibi harusi akimkatia keki mumewe...Ama kweli dunia inaelekea mwisho




Wednesday, October 7, 2009

Miss wetu, Miss Tanzania 2009, Miriam.

Huyu ndiye Miss Tanzania Wetu 2009! Anaitwa Miriam Gerald kutoka mwanza, aliyetwaa taji la Miss Tanzania baada ya Kuwashinda wenzake 28. Hapo juu akipungia baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya gari aina ya Suzuki Grand lenye thamani ya Shilingi milioni 54.
Miriam alizaliwa mwaka 1987 na kuanza elimu ya msingi katika shule ya msingi Lake huko huko jijini mwanza na kumaliza elimu yake ya msingi mwaka 2000. Baada ya hapo alijiunga kidato cha kwanza katika Shule ya sekondari Thaqafa na kumaliza kidato cha nne mwaka 2006 kabla ya kujiunga na shule ya sekondari Taqwa kwa elimu ya kidato cha tano na sita na kuhitimu mwaka 2006. Kwa sasa anafanya kazi katika kampuni ya simu Vodacom upande wa huduma kwa wateja.

Hapo juu, warembo, akiwemo Miriam,(Wa pili kutokea kushoto.), wakipita na Vazi La Ufukweni.

"Kila mmoja alikuwa akihema kwa presha. Akaanza kuitwa Julieth William kama mshindi wa tatu, mapigo ya moyo wangu yaliendelea kuwa juu, nilipowaaangalia wenzangu niligundua walikuwa na tatizo kama langu. Akafuatia Beatrice,matumaini yakaanza kufifia kidogo, lakini bado nikajipa moyo wakati huo wale wenzangu waliendelea kusubiri. Usisikie ukiwa huku nyuma ya pazia, roho inadunda sana. Nilibaki mimi Sylvia na Sia. Nikawa naangalia juu, huku kila mmoja akimtizama mwenzake. Jaji akaanza kutangaza, ' The winner of Vodacom Miss Tanzania 2009 is......contestant number zero three...Miriam Gerlad'. Unajua sikuamini, nikasema mungu wangu, nikahisi kama kuchanganyikiwa, nikanyanyuka na kuanza kufurahi ndani kwa ndani...." Hayo yote ni maneno toka mdomoni mwa Miriam akielezea hali aliyokuwa nayo kabla na baada ya Kuwa Miss Tanzania 2009.
..................................................................

ELIZABETH NAYE AENDELEA NA BIG BROTHER YAKE!!
Mshiriki wa Tanzania katika shindano la Big Brother Africa Elizabeth Gupta bado ameendelea kuwa kin'gan'ganizi katika shindano la Big Brother linaloendelea huko nchini Afrika kusini huku tayari washiriki kadhaa wakiwa wameshatolewa katika jumba hilo.

Pichani akiwa ndani ya Jumba hilo na washiriki wenzake.

Hapa akiwa jikoni akifanya mambo ya maankuli, sijui alikuwa anawapikia ugali!!!!!!
............................................................

VIJIMAMBO VYA AUNT EZEKIEL,MISS NA PIA TZ MOVIE STAR.
Aunt Ezekiel si jina geni kwa masikio ya wengi. Alianza kujulikana kupitia mashindano ya urembo, hapa nazungumzia katika mchakato wa kumpata Miss Tanzania mwaka 2006.
Kama ilivyo ada ya shindano huanzia katika kitongoji, then mkoa, then kanda kabla ya kumalizikia kitaifa, hali kadhalika Aunt Ezekiel alipitia kote huko. Alianzia kitongoji cha Ilemela akaibuka mshindi, ushindi uliompa nafasi ya kushiriki Miss Mwanza ambako pia alikuwa nambari wani.
Tiketi ya Miss Mwanza ilimpa nafasi ya Kushiriki Miss kanda ya Ziwa ambako alishika nafasi ya pili kigezo kilichompa sifa ya moja kwa moja kushiriki Miss Tanzania Level ya kitaifa ingawa hakufanya vizuri sana ingawa si vibaya sana kwani angalau alifanikiwa kuingia kumi bora.

Baada tu ya mashindano ndipo umaarufu wake ulipoanza kustawi maradufu, lakini hiyo ilikuwa ni baada ya kuangukia kwenye penzi la Pendejee maarufu hapa mjini Jack Pemba. Kilichomfanya awe maarufu ni Life Style yao iliyotawaliwa na vituko na matukio ya kila aina kiasi cha kusababisha kila kukicha apambe kurasa za mbele za magazeti hususan ya udaku, kitu kilichomfanya afahamike kila kona.
Baada ya kuachana na Jack Pemba akaangukia kwenye mikono ya mtu mwingine maarufu, Hartman, mmiliki wa Hartman Records. Bado aliendelea kupata skendo na kuendelea kupamba magazeti kila siku kutokana na uhusiano wake huu mpya kwani Hartman ni mume wa mtu hivyo ikawa ni Skendo kila kukicha. Umaarufu ukazidi!!

Aunt Ezekiel alianza shule ya msingi mwaka 1992 pale shule ya msingi Bunge jijini Dar Es Salaam na kumaliza darasa la Saba mwaka 1999. Mwaka 2000 alijiunga kidato cha kwanza na kumaliza mwaka 2004. Bahati mbaya hakuweza kuendelea tena na elimu baada ya hapo.
Ndipo alipojiingiza kwenye Modelling, safari ndefu iliyomfikisha kwenye kushiriki hadi Miss Tanzania mwaka huo wa 2006.
Baada ya umaarufu wa Modelling na mengineyo, sasa Aunt Ezekiel amejikita zaidi kwenye uigizaji na kama ni mfuatiliaji mzuri wa filamu za kibongo utakubaliana nami nikishasema kuwa ameshacheza muvi nyingi sana zisizo na idadi nafikiri hata ukimuuliza mwenyewe atakuwa amezisahau kadhaa. Lakini muvi yake ya kwanza kabisa kuicheza iliitwa Miss Bongo part 1 & 2, iliyotoka chini la Lebel ya Game 1st Quality. Huyo ndio Aunt Ezekiel, kama hapo juu anavyoonekana na Mr Chuz katika filamu ya Hostel..









Tuesday, October 6, 2009

Mambo ya Ulaya Ulaya!!!

Rihanna amefanya kituko cha ajabu baada ya kutinga kwenye mnuso mmoja huku akiwa ametinga kigauni kinachoonyesha sehemu adimu za ndani ya mwili wake.(Tazama picha hapo juu). Kigauni hicho kilionyesha wazi maziwa yake, kitovu, na sehemu fulani fulani muhimu (Ngumu kuzitaja). Haikueleweka mara moja alikuwa na nia gani, ujumbe gani kwa fans wake au ilikuwa ni mambo fulani ya Fashion tu. Anyway sio issue, alipendeza lakini!
..................................................................................

Will Smith na mkewe Jada Pinket Smith, wametajwa kuwa ndio watakuwa waongozaji wa sherehe za tuzo za amani za Nobel,(Nobel Peace Prize), zinazotegemewa kufanyika mwaka huu mjini Oslo nchini Norway, tarehe 10 Desemba.
Tuzo hizi ambazo hufanyika kila mwaka, huwa ni maalumu kwa ajili ya kutoa heshima au kutuza watu ambao wametoa mchango mkubwa kusaidia amani ya dunia, na Will Smith na mkewe wanasema hii ni fursa ya pekee na heshima kubwa kwao kuongoza sherehe hizo.
Wasanii mbali mbali wamealikwa kutumbuiza sherehe hizo ambao ni pamoja na Wyclef Jean, Toby Keith, Donner Summer, Louis Fonsi na Amadou and Marian.
Kwa mujibu wa ripoti, Raisi wa marekani Barack Obama na Rais wa Ufaransa Nicolous Sarkozy ni kati ya watu 205 waliochaguliwa kugombea tuzo hiyo kwa mwaka huu.!! Lakini pamoja na yote, hebu cheki hilo pozi hapo juu la Will Smith na mkewe, ndoa tamu eeh!! Lakini iwe na amani!
.........................................................................................
Gar ya ajabu hapo juu linaitwa Batmobile, limetengenezwa na jamaa mmoja hivi huko nchini Sweeden. Mpaka kukamilika kwake lilitumia dola za Kimarekani milioni moja na pia ilitumia muda wa miaka mitatu na nusu mpaka kukamilika kwake. Ndani yake ina Sattellite Navigation system, kitambua sauti, machine guns, Camera kwa ajili ya Ulinzi wake binafsi, DVD Players, Plasma TV na kitufe kwa ajili ya kucontrol urefu wake. Ukitaka liwe fupi sana sawa, ukitaka liwe refu sana sawa. Kazi kwenu wadau, wewe mwenye Hummer na mimi nikiwa na hili nani atakuwa zaidi?
................................................................................


Lalla Drogba ambaye ni mke wa mchezaji maarufu wa Chelsea ya uingereza amabaye ni raia wa Ivory Coast, Didie Drogba, ameibuka na kudai kwamba yeye ni matawi ya juu kabisa kuliko mpenzi wa mchezaji yoyote yule wa Uingereza.
"Mimi ni zaidi ya mwanamke wa mchezaji yoyote yule unayemjua hapa uingereza. Maana nina kila kitu ambacho mwanamke anatakiwa kuwa nacho hususani elimu, jambo ambalo wanawake wengi wa wachezaji wa hapa hawajasoma kama mimi." Alijigamba Lolla.
Lakini kuna ukweli ndani yake katika kauli hii kwani mwanadada ana taaluma ya sheria na ni mwanadiplomasia ambaye anafanya kazi katika shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia wakimbizi (UNHCR.)
Lolla na mumewe Drogba,(Pichani juu.) wana watoto wanne tayari mpaka sasa, watatu wakiwa wa kike na mmoja wa kiume. (Huyo wa kiume ningekuwa mimi ningemuita Epharaim!!)
........................................................................................



Mwanamuziki Fifty Cent ametoa hewani mwonekano wa albamu yake mpya ya Before I Self Destruct (Official Cover for Before I Self Destruct Album.), ambayo inatarajiwa kuwa dukani tarehe 17/11/2009. Hapo juu ndio jinsi Cover la album hiyo lilivyo.